.


  Wanaowajibika kutowa

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Wanaowajibika kutowa

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:10 pm

  Wanaowajibika kutowa

  Wanaowajibika kutowa

  · Muislam anayemiliki Niswaab, nacho ni 'Kiwango maalum cha mali kilichowekwa na sheria katika aina yoyote ile ya mali inayowajibika kuitolea Zaka.

  · Niswaab hiyo lazima iwe ishatolewa ndani yake mahitajio ya dharura ya lazima kama vile chakula, mavazi, makazi, vyombo vya nyumbani, chombo cha usafiri na vyombo vyake vya kufanyia kazi, madeni nk.

  · Lazima kiwango hicho kiwe kimemilikiwa kwa muda wa mwaka mzima (mwaka wa Kiislam) bila kupungua katika wakati wowote ule ndani ya mwaka huo, na kama kitapungua katika wakati wowote ule kabla ya kutimia mwaka, basi hesabu nyingine mpya itaanzwa kuanzia pale kinapokamilika tena Kiwango hicho.

  Amesema Imam An Nawawiy:

  "Madhehebu yetu na madhehebu ya Maimam Malik na Ahmad na ya maulamaa walio wengi ni kuwa; Mali inayotolewa Zaka kwa ajili yake, kama vile dhahabu, fedha na wanyama wa kufugwa, lazima kiwango chake kibaki kwa muda wa mwaka mzima bila kupungua. Na wakati wowote ule kitakapopungua, basi mwaka wake unakatika, na wakati wowote ule kitakapotimia tena, unaanza kuhesabiwa mwaka mwingine".  Abu Hanifa anasema:

  "Kinachotakiwa ni kuwepo kwa Kiwango (Niswaab) mwanzo wa mwaka na mwisho wake, na haidhuru iwapo kitapungua katikati ya mwaka, hata kama mtu alikuwa nazo Dirham mia mbili kisha zikapotea zote katikati ya mwaka na akabakiwa na dhirham moja tu, au kama alikuwa na kondoo arubaini wakapungua na akabaki mmoja tu, kisha mwisho wa mwaka akaweza kumiliki (Dirham) mia mbili kamili au (kondoo) arubaini kamili, basi itawajibika Zaka kwa vyote".  Masharti haya hayahusiani na Zaka za mazao na matunda, kwa sababu vitu hivyo Zaka yake inatolewa siku ya mavuno.

  Mwenyezi Mungu anasema:

  أَثْمَرَ وَآتُواْ حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ

  "Na toeni haki yake siku ya kuvuna kwake".

  Al An-am – 141

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 1:32 pm