.


  Kuidhihirisha Zaka

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Kuidhihirisha Zaka

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:13 pm

  Kuidhihirisha Zaka

  Inazuju kwa mtoaji kuidhihirisha au kuitoa kwa siri Zaka yake, yote sawa ikiwa anachokitowa ni Sadaka ya kawaida au Zaka ya mali, ingawaje kuitoa kwa siri ni bora zaidi.

  Mwenyezi Mungu Anasema:

  إِن تُبْدُواْ الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاء فَهُوَ خَيْرٌ لُّكُمْ

  "Kama mkitoa sadaka kwa dhahiri ni vizuri, na kama mkitoa kwa siri na kuwapa mafakiri, basi huo ni ubora zaidi kwenu".

  Al Baqarah - 271  Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

  "(Watu aina) Saba Mwenyezi Mungu atawaweka chini ya kivuli chake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake:- Imamu muadilifu, na kijana aliyekulia katika kumuabudu Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umeshughulika na misikiti, na watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, walikutana kwa ajili Yake na wakafarikiana kwa ajili Yake, na mtu aliyetoa Sadaka kwa siri akaificha hata (mkono wake wa) kushoto usijuwe nini kimetolewa na wa kulia, na mtu aliyemtaja Mwenyezi Mungu akiwa peke yake mpaka akatoka machozi, na mtu aliyeitwa na mwanamke aliye na cheo (kikubwa) na mali (nyingi) akimtaka kwa ajili ya nafsi yake (akimtaka azini naye), akasema (mtu huyo); "Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu".

  Bukhari - Muslim na Imam Ahmad

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 1:12 pm