.


  Kuisafirisha Zaka

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Kuisafirisha Zaka

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:15 pm

  Kuisafirisha Zaka

  Mulamaa wengi wamekubali kuwa mali ya Zaka (Zakatul Maal - si Zakatul Fitr) inaweza kusafirishwa na kutolewa katika nchi nyingine kwa wanaoistahiki zaidi ikiwa watu wa mji anaoishi mtoaji hawaihitajii zaidi mali hiyo. Ama ikiwa katika nchi hiyo wapo wanaoihitajia, basi zipo hadithi zinazotujulisha kuwa Zaka ya kila nchi wanapewa masikini wake.

  Katika madhehebu ya Imam Abu Hanifa, wao wanasema:

  "Ni Makruh kuisafirisha mali ya Zaka isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kumsaidia ndugu wa nasaba mwenye kuihitajia, na hii inatokana na umuhimu wa kuunganisha undugu huo, au pia kwa ajili ya watu wenye shida sana katika watu wa nchi yake, au kwa ajili ya kuiondoa kutoka nchi ya kikafiri na kuipeleka katika nchi ya kiislam."  Madhehebu ya Imam Shafi yanasema:

  "Haijuzu kuisafirisha mali ya Zaka na inawajibika kutolewa katika nchi iliyochumwa mali hiyo isipokuwa pakikosekana wenye kuihitajia Zaka hiyo katika nchi hiyo".  Muadh bin Jabal (Radhiya Llahu anhu) alipewa ugavana wa nchi ya Yemen na Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam), na alipotawala Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) alimuacha Muadh aendelea kuwa gavana wa nchi hiyo. Lakini Muadh (Radhiya Llahu anhu) alipompelekea Umar bin Khattab (Radhiya Llahu anhu) theluthi ya mali ya Zaka, Umar (Radhiya Llahu anhu) alikataa kuzipokea akamwambia:

  "Sikukupeleka uwe mchotaji (wa mali) wala mpokeaji wa kodi, bali nimekupeleka kwa ajili ya kuchukua mali (ya Zaka) kutoka kwa matajiri wao na kuzirudisha kwa masikini wao".

  Muadh (Radhiya Llahu anhu) akasema:

  "Nisingekuletea ila kwa sababu sikumpata (masikini) anayezistahiki kuzichukua".

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 1:54 pm