.


  Watu wema

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Watu wema

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:17 pm

  Watu wema

  Zaka anapewa Muislam anayeistahiki akiwa Muislam huyo ni mtu mwema au mtu asi, isipokuwa mtu asi hapewi kaika mali ya Zaka ikiwa itajulikana kwa uhakika kuwa atakuja kuitumia mali hiyo katika kuuendeleza uasi wake.

  Ikijulikana kwa uhakika kuwa ataitumia mali hiyo katika kumuasi Mwenyezi Mungu, basi mtu huyo atanyimwa, ama ikiwa hayajulikani hayo, au ikijulikana kuwa ataitumia mali hiyo katika shida zake, basi hapo atapewa.

  Hata hivyo ni bora kwa mtoaji Zaka aihusishe mali hiyo kwa kuwapa watu wema au maulamaa wanaostahiki wanaoifayia kazi elimu yao, kwani Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

  "Walisheni chakula chenu wachaMungu na mnaowajuwa katika walioamini (kweli)".

  Ahmad  Anasema Ibni Taymiya:

  "Asiyeswali hapewi katika mali ya Zaka mpaka pale atakapotubu akawa anaswali."  Anasema Sayed Sabeq:

  "Katika kundi hilo wanaingia pia wale wanaomuasi Mwenyezi Mungu bila kujali wala kuona haya, na kuendelea kuzama katika maasi huku nyoyo zao zikiwa zishafisidika na dhamiri zao zimekwisha haribika".  Hawa hawapewi katika mali ya Zaka isipokuwa kama Zaka hiyo itawasaidia katika kuwaongoza mwongozo ulio sahihi au itawasaidia katika kutoka hali yao hiyo.

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 12:59 pm