.


  Walioharimishwa kupewa

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Walioharimishwa kupewa

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:22 pm

  Walioharimishwa kupewa

  1. Kafiri

  Katika hadithi iliyotangulia, Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

  "Zichukuliwe kutoka kwa matajiri Wao na kurejeshewa masikini Wao"

  Na maana yake ni kuwa:-

  Zichukuliwe kutoka kwa matajiri wa Kiislam na kupewa masikini wa Kiislam.  2. Bani Hashim

  Nao ni watoto wa Aliy na Aqiyl na Jaafar na Al Abbas na Al Harith (Radhiyallahu anhum).

  Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema:

  "Sadaka haijuzu kupewa kwa watu wa Muhammad".

  Muslim  Maulamaa wamekhatalifiana juu ya ukoo wa Bani Al Muttalib, iwapo nao pia hawapewi katika mali ya Zaka au wanapewa.

  Imam Shafi amesema kuwa hawa nao wasipewe katika mali ya Zaka, na hii inatokana na hadithi iliyotolewa na Imam Shafi na Imam Ahmad na Imam Bukhari kutoka kwa Jubair bin Mut-am aliposema:

  "Siku ya Khaibar (baada ya kumalizika vita hivyo), Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliikusanya upande mmoja sehemu ya ngawira ya watu wa ukoo wake katika Bani Hashim na ya Bani Al Muttalib na akawaacha (watu wa kabila lake) katika Bani Nofel na Bani Abdu Shams. Tukamwendea mimi na Uthman bin Affan na kumuuliza:

  "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hawa ni Bani Hashim na sisi hatukanushi fadhila zao kutokana daraja yako mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini vipi hawa ndugu zetu katika Bani Al Muttalib, umewaingiza wao ukatuacha sisi wakati nasaba yao na yetu juu yako ni sawa sawa?"

  Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) akasema:

  "Sisi na Bani Muttalib hatujafarikiana katika ujahilia wala katika Uislam, bali sisi na wao ni kitu kimoja". Akaviingiza vidole vyake vya mkono wa kulia ndani ya vidole vya mkono wa kushoto na kuvichanganya."  Kutokana na ushahidi huu, baadhi ya maulamaa wakasema;

  'Bani Muttalib nao pia wanaingia katika kuharamishiwa kupewa katika Mali ya Zaka".  3. Baba na watoto

  Haijuzu mtu kumpa katika mali ya Zaka baba yake, mama yake, watoto wake na babu zake, na hii ni kwa sababu mtoaji Zaka anawajibika kuwatizama watu hao na kuwapa katika mali yake, na kwa ajili hiyo, watu hao wanalazimika kuwa matajiri kutokana na utajiri wake.  4. Mke

  Haijuzu mtu kumpa mkewe katika mali ya Zaka, na jambo hili linakubaliwa na maulamaa wote na hii ni kwa sababu mtu anawajibika kumtizama na kumpa mkewe katika mali yake kama anavyowajibika kuwapa wazee wake wawili akiwa anao uwezo huo.

  Anasema Ibnil Mundhir:

  "Isipokuwa kama mke ana deni, basi hupewa Zaka katika ile sehemu ya kuwasaidia wenye madeni kwa ajili ya kulipa deni hilo".

  Ama ikiwa mke ni tajiri mwenye uwezo wa kutoa Zaka, basi yeye anarushusiwa kumpa mumewe katika mali ya Zaka kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) aliposema:

  "Amesema kweli Ibni Masaud, mumeo na mwanao wanastahiki zaidi kuwapa Sadaka".

  Bukhari  5. Haijuzu kuitumia mali ya Zaka kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kama vile kujenga misikiti, kununua misahafu, kununua vifaa vya kusaidia kuosha maiti nk. Na hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu kwa hekima yake keshazitaja na kuzisherehesha njia za kutoka Zaka katika aya iliyotangulia ya Surat At Tawba -60, na akaikamilisha aya hiyo kwa kusema;  "Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 1:01 pm