.


  Wanaostahiki Zaka

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  Wanaostahiki Zaka

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 12:26 pm

  Wanaostahiki Zaka

  Sadaka ya kawaida, anapewa mtu yeyote hata akiwa si Muislam, ama Zakatul Fitri wanapewa watu wa aina mbili tu, nao ni masikini na mafakiri Waislam.

  Zakatul Maal (Zaka ya mali), hii wanapewa aina 8 tu ya Waislamu waliowataja na Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu Aliposema:

  إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاء وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ فَرِيضَةً مِّنَ اللّهِ وَاللّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

  "Sadaka hupewa (watu hawa):-

  · Mafakiri na

  · Masikini na

  · Wanaozitumikia na

  · Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislam) na

  · Katika kuwapa uungwana watumwa na

  · Katika kuwasaidia Wenye deni na

  · Katika (kutengeneza) Mambo aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na

  · Katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa).

  Ni faradhi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".

  At Tawaba - 60.  Ayakayeichunguza aya hii ataona kuwa Mwenyezi Mungu ametumia neno 'Lil' katika kuwataja watu aina nne wa mwanzo wanaostahiki kupewa Zaka. Na hii inaitwa Laam ya tamliyk, na maana yake ni kuwa lazima kuwamilikisha watu wa aina nne wa mwanzo (yaani kuwapa mikononi mwao) Zaka yao.

  Mwenyezi Mungu ِAnasema:

  إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاء وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ

  Ama katika aina nne waliobaki, Mwenyezi Mungu ametumia neno 'Fiy'. Na kwa kutumia neno hilo Mwenyezi Mungu hatulazimishi, kuwamilikisha kwa kuwapa Zaka yao mikononi mwao.

  Mwenyezi Mungu anasema:

  وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ

  Kwa hivyo katika aina nne za mwisho, kwa mfano kama unataka kumsaidia mwenye deni, hulazimiki kumpa pesa hizo mkononi mwake, bali unaweza kwenda kumlipia deni hilo moja kwa moja bila ya kumkabidhi mdaiwa huyo pesa hizo mkononi mwake. Hata hivyo, ukitaka unaweza pia kumkabidhi mweyewe mkononi mwake.

  Ukitaka kuzitumia pesa za Zaka katika njia ya Mwenyezi Mungu, unaweza kununua kwa mfano silaha na kuwakabidhi wapiganaji 'Mujahidiin' au unaweza kuzitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu bila ya kumkabidhi mtu pesa hizo mkononi mwake, wakati huo huo unaweza ukitaka kuwakabidhi wanaohusika au wajuzi ili ipate kutumika kwa usahihi zaidi.

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 12:54 pm