.


  MILA ZINAZOPINGANA NA KUKHALIFIANA NA SHERIA

  Share
  avatar
  Admin
  Admin

  Posts : 22
  Join date : 2010-08-28
  Age : 36
  Location : london

  MILA ZINAZOPINGANA NA KUKHALIFIANA NA SHERIA

  Post  Admin on Mon Aug 30, 2010 8:51 pm

  MILA ZINAZOPINGANA NA KUKHALIFIANA NA SHERIA

  Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia ndani ya Qur-ani Tukufu:"ENYI MLIOAMINI !INGIENI KATIKA HUKUMU ZA UISLAMU ZOTE, WALA MSIFUATE NYAYO ZA SHETANI, KWA HAKIKA YEYE KWENU NI ADUI DHAHIRI".

  Hili nitangazo na agizo la Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kila ambaye ameukiri na kuukubali uislamu kwa khiyari yake mwenyewe. Katika tangazo na amri hii analazimishwa kila muislamu kuufuata uislamu mzima kama mfumo wa maisha yake yote. Aufuate uislamu katika maisha yake ya kijamii, kiuchumi,kielimu, kiulinzi, kiibada na baki nyanja nyingine za maisha yake. Atambue kuwa uislam kama dini ndio mfumo sahihi wa sheria, mila na utamaduni umfaao mwanadamu. Ni mfumo ulio kamilika, kwa mantiki hii uislamu,uislamu hauna upungufu na wala hauhitajii ziada yoyote kutoka popote pale. Haya yanathibitishwa na kauli tukufu ya Mola Mtukufu: "LEO NIMEKUKAMILISHIENI DINI YENU, NA KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU, NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI YENU…."[5:3]

  Aya inaeleza bayana kuwa uislamu ndio mfumo sahihi na kamili wa maisha, uislamu ni Neema ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu kwa waja wake uislamu ndio dini TEULE na CHAGUO la Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake. Kwa mantiki hii, leo waislamu kuhukumiana nje ya Qur-ani , kufuata mila na tamaduni zinazokhalifiana na sheria ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu ni sawa na kuibatilisha aya hiyo hapo juu isemayo kuwa uislamu umekamilika. Matendo yao hayo yanaonyesha kuwa uislamu umesahau kuyawekea sheria, kanuni na taratibu baadhi ya maeneo katika maisha ya mwanadamu. Kwa hivyo, wao wanayo fursa ya kujipangia sheria, kanuni na taratibu zitakazokidhi haja zao katika maeneo husika bila kujali wala kuangalia kuwa kanuni na taratibu hizo zinapingana na sheria ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu na isitoshe bado watu hawa waliojiundia mila na tamaduni zao nje ya uislamu bado wanadai na kujiita kuwa ni waislamu. Mtu ana khiyari ya ama kuwa au kutokuwa muislam, kwa ushahidi wa kauli yake Mwenyezi Mwenyezi Mungu Mtukufu : "HAKUNA KULAZIMISHWA (mtu kuingia)KATIKA DINI UONGOFU UMEKWISHA PAMBANUKA NA UPOTEFU BASI ANAYEMKATAA SHETANI NA AKAMWAMINI ALLAH BILA SHAKA YEYE AMESHIKA KISHIKO CHENYE NGUVU KISICHOKUWA NA KUVUNJIKA…"[2:256]

  Na akasema tena : "NA SEMA : "HUU NI UKWELI ULOTOKA KWA MOLA WENU BASI ANAYETAKA NAAMINI NA ANAYETAKA NA AKUFURU …."[18:29]

  Mtu akishautumia uhuru na khiyari aliyopewa na akauchagua uislamu kama dini na mfumo wa kuyatawala maisha yake yote, hapo sasa hana khiyari tena ya kuchagua hukumu/sheria zipi za uislamu asifuate na zipi asizifuate, bali analazimishwa kuzifuata shria zote. Mwenyezi Mungu Mtukufu anaikemea vikali tabia hii ya kufuata baadhi ya hukumu/sheria na kuacha nyingine, tusome na kutafakari : "… JE! MNAAMINI BAADHI YA KITABU NA KUKATAA BAADHI (yake) ? BASI HAKUNA MALIPO KWA MWENYE KUFANYA HAYA KATIKA NYINYI ILA FEDHEHA KATIKA MAISHA YA DUNIA ; NA SIKU YA KIYAMA WATAPELEKWA KATIKA ADHABU KALI …."[2:85]

  Mwenyezi Mungu Mtukufu anazidi kutuambia na kutuonyesha kuwa Muislamu wa kweli hana khiyari, uhuru wala uchaguzi katika kufuata ama kutokufuata sheria/hukumu za kiislamu kama mfumo sahihi wa maisha, tusome na tuzingatie: "HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI, WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO, NA MWENYE KUMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI(kabisa)". [33:36]

  Mpaka hapa, tayari tume kwisha thibitisha kuwa uislamu ni dini iliyokamilika na kwamba mwislamu hana uchaguzi katika kufuata ama kutokufuata hukumu/sheria za uislamu.

  Muislamu hana fursa hata kidogo ya kujiundia kanuni, taratibu, mila au desturi na ada zilizo nje ya uislamu, kitendo hicho ni kosa kubwa ambalo limeandaliwa adhabu kali iumizayo na kutia uchungu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hebu sasa tujaribu kuziangalia baadhi ya mila, tamaduni, desturi na ada zinazokhalifina na kupingana na sheria. Desturi na ada hizi tunazoishi nazo kataka jamii na kurithishana kizazi hata kizazi zimezoeleka na kuota mizizi katika jamii zetu kiasi cha kusifanya zionekane kuwa ni za kawaida na zinakubalika katika dini, na ukweli ni kwamba hazina nafasi kabisa katika dini hii iloyokamilika na kujitosheleza.

  UNYAGO

  Hii ni mila na desturi iliyoenea na kufuatwa na makabila mengi khusasan hapa kwetu Tanzania. Unyago ni mila ya kumcheza mtoto wa kike wakati avunjapo ungo. Wakati huo huandaliwa ngoma maalum ambayo huwashirikisha akina mama watu wazima. Hawa kazi yao kubwa ni kile kinachoitwa "kumfunda" mwanamwali, yaani kumfahamisha kuwa sasa yeye amekuwa mwanamke na kumealeza nafasi yake kama mwanamke, majukumu yake na jinsi ya kuishi na mume. Ngoma hii huchezwa mahala pa wazi, mahali ambapo hata mwanamume hupata fursa ya kuwaona wanawake, wake za watu wakikata viuno. Mahala hapa, mwanamwali huonyeshwa akiwa kavishwa khanga ya kiuno tu na baki ya mwili wake kuachwa wazi ikiwa ni pamoja na matiti yake. Katika ngoma hii wanawake hunywa pombe ili kutoa aibu na haya wapate kukata viuno vizuri, na baadhi au wengi washirikio katika mila hii hujiita kuwa ni waislamu. Waelewe uislamu hakuna mila kama hizi mbaya na kushikilia kuzifuata na kuziendeleza desturi hizi huku wakivaa vazi la uislamu, huko ni kuudhalilisha na kuutukanisha uislamu. Mila na desturi hizi huzifai kwa kuwa zinapingana na sheria kamilifu ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu, kwa hivyo tuziache mara moja pamoja na kuzizoea na kuzionea ladha kwetu. Mila hizi hazifai kwa sababu zifuatazo:

  1. Unyago huwashirikisha mwanaume na wanawake, kama tushuhudiavyo leo. Katika uislamu ni kosa kubwa mwanamume kuchanganyika na wanawake.
  2. Katika unyago huimbwa nyimbo za matusi, hili halikubaliki hata kiakili na kimaadili seuze sheria .
  3. Katika unyago watu hulewa eti kwa sababu ya kumsherekea mtoto wao. Uislamu umekataza ulevu kwa sababu yoyote ile iwayo, hata kama ni dawa kama wanavyodai hivyo baadhi ya watu.
  4. Mwanamwari hudhalilishwa na kunjiwa heshima yake kama mwanadamu kwa kuanikwa uchi mbele ya hadhara ya watu wakiwemo mwamume.
  5. Katika unyago hupatikana matumizi mabaya ya mali. Pesa ambazo zingetumika katika mambo mengiya maendeleo kwa maslahi ya jamii na familia husika, hutumika kununulia pombe, kuwalipa wapiga ngoma na kugharimia chakula cha wanangoma kwa kipind chote cha ngoma. Hii ndio israafu inakemewa na kukatazwa na uislamu.

  Kwa ujumla, huzalikana na kupatikana katika desturi na mila hii ya unyago, mambo mengi ambayo yanakhalifiana na sheria. Kwa mantiki hii kila aliyekuwa muislamu anpaswa kuziacha mara moja mila na desturi hizi ili awe muislamu kamili.Uislamu haupingi wala kulikataa suala la kumfundisha mtoto wa kike/kiume nafasi yake yeye kama mwanamume/mwanamke na majukumu yake kama mke kwa mumewe au mume kwa mkewe. Aishi vipi na jamii, ailee vipi familia. Uislamu unapinga na kukataa namna au njia na jinsi itoleavyo elimu hii. Uislamu umesheheni fani zote za elimu iwe na elimu ya kijamii, uchumi, afya, ulinzi na usalama, siasa na kadhalika, zote hizi zimo ndani ya uislamu, tusome tu tutakutana nazo. Sasa kama elimu hii tunayo, kwa nini hatujifunzi na kuitoa kwa misingi yetu ya kiislamu?! Jamani , tuziache mila, desturi na ada hizi potofu na badala yake tushikamane na kuifuata mila na desturi sahihi za uislamu. Uislamu ndio mila baba yetu Nabii Ibrahimu- Rehema na Amani zimshukie, tusome: "…..(Nayo dini hii) NI MILA YA BABA YENU IBRAHIMU…."[22:78]

  Hivi ni kweli kuwa leo sisi tunaweza kuwa na mila na desturi bora kuliko mila ya Nabii Ibrahimu?! Kuacha kufuata mila ya Baba yetu Ibrahimu na kujiundia mila zetu wenyewe huo ni UPUMBAVU, tusome na tukubali: "NA NANI ATAJITENGA NA MILA YA IBRAHIMU ISPOKUWA ANAYEITIA NAFSI YAKE KATIKA UPUMBAVU…"[2:130]

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 12:34 pm