.


  UFAHAMU WA SURA AL-KAFIROON

  Share
  avatar
  essam

  Posts : 3
  Join date : 2010-08-28
  Age : 34
  Location : dublin

  UFAHAMU WA SURA AL-KAFIROON

  Post  essam on Sat Aug 28, 2010 9:03 am

  TAFSIRI YA SURAT AL-KAFIROON.

  Sabau ya kuteremshwa

  Qur-aan imeteremshwa ili iwe ni muongozo kwa binaadamu wote, wakati wowote na matokeo yote yatakayo tokea. Ijapokuwa baadhi ya aya ziliteremshwa kwa matokeo maalumu, wakati maalum katika historia. Neno la kiarabu “sabab” (wingi-asbab) inamaana ya sababu, kisa na neno la “maarifat asbab al-nuzul” inamaana ya ufahamu, ujuzi kuhusu tokeo maalum katika historia inayohusiana na materemsho maalum katika Qur-aan.

  Mwanazuoni maarufu wa somo hili Wahid ameandika kuwa “Ufahamu wa tafsiri ya Qur-aan haupatikani bila ya mtu kujihusisha zaidi na historia na sababu ya kuteremshwa kwa aya (d.468/1075) kitabu (asbab al-nuzul) cha Al-Wahid al-Nisaburi-Cairo –1968-p4.

  Ujuzi wa ufahamu wa sababu ya kuteremshwa kwa aya unasaidia katika kufahamu hali halisi iliyo iliteremshwa aya, ambao ndio mwangaza wa utimizaji wa ujumbe huo na humpa mtu muongozo katika kuelezea tafsiri na utekelezaji wa vitendo wa aya hizo katika masuala tofauti.

  Kwa kufuata ufahamu huu, andiko hili litatuelezea ufahamu wa surat- Al-Kafiroon na juu ya ufuataji wake kwa vitendo katika wakati wetu huu.

  Asbab ul-Nuzul ya Surah Al-Kafiroon.

  Hii ni moja kati ya surah zilizoteremshwa Makka kwa Mtume wa Mwenyezi Mung (saw) katika kipindi cha kampeni ya ulinganiaji wa Mfumo wa maisha ya Kiisilamu. Vitabu vya hiztoria vinaeleza kuwa baada ya Makafiri kubaini athari za ujumbe huo wa Uisilamu umekuwa na wafuasi wengi, walianzisha njia tatu kuu juu ya kusimamisha wito huo. Njia hizo zikiwa ni mateso makali, upotevu wa ujumbe na uzuifu wa chakula kwa wafuasi wake.

  Mfasiri Ibn Kathiri kaeleza katika tafsiri yake ya Qur-aan kuwa, Makuraishi walitaka kuwepo na muafaka baina yao na Mtume (saw), na wakapendekeza kuwa Mtume (saw) awabudie Miungu yao kwa kipindi fulani na wao wataabudu Mungu wake kwa kipindi hicho, kisha asimamishe kulingania wengine kufuata dini yake na kuwasimangia Miungu yao na mfumo wao wa Kimaisha, kwa malipo ya kumpa chochote atakacho dai kutoka kwao mf. mali, wake, ufalme n.k.

  Makuraishi waliona kuwa mfarikiano baina yao na Mtume ulikuwa ni mkubwa, hivyo pendekezo lao la muafaka walihisi ni wa haki kwa upande wao na kwa upande wa Mtume ili waishi kwa amani.

  Kwa kufupisha kisa hicho na kubainisha tofauti ya imani za pande zote mbili, sura hii Al-kafiroon iliteremshwa kwa kueleza na kubainisha kuwa haiwezekani kabisa Islam (Tauheed) na Ukafiri (shirk) kuchanganyika pamoja.

  TAFSIRI YA SURA.

  Sura imeelezea kwa uwazi tofauti iliyopo kati ya Shirki na Tauheed, kwa maneno yaliyotumika katika sura hii na kuonesha kuwa tofauti hiyo haikuwekwa na binadamu bali nikutoka kwa Muumba na ni amri yake Mola.

  “Qul” “sema” ni neno ambalo linaonesha wazi kuwa ni amri kutoka kwa mola kumuamrisha Mtume aseme kuwaambia makafiri hayo yanayofuatia mbele ya aya hiyo, na kuonesha kuwa mambo yote ya dini na kimaisha ni yake Allah na yeye ndiye muamuzi na muamrishaji juu ya maisha ya binadamu.

  Allah (s.w) amemuongoza Mtume jinsi ya kuwajibu makafiri kwa kutumia jinsia yao halisi ya ukafiri.

  “Sema enyi makafiri” (Kafiroon:1)

  Ibn Kathiri kasema kuwa “makafiri” kila yule ambaye asiye amini juu ya uislam katika ulimwengu huu. Wale wote wasiofuata dini iliyoteremshwa na mola na wote wasiomuamini Mtume. Na hakuna kinachotukutanisha baina yetu na wao popote tulipo. Kwa hivyo tunaona mwanzo wa sura kuwa inajenga katika akili kuwa uwazi tofauti ambayo haiwezi kufichika au kukatalika (baina ya tawheed na shirk).

  “Siabudu munavyoabudu” (Kafiroon:2)

  Ni tamko ambalo limesisitizwa kwa kurejewa kuwa

  “Na sito abudu kabisa mnavyoabudu”.(Kafiroon:4)

  “Nanyi wala hamuabudu ninayemuabudu”.(Kafiroon:5)

  Pia ujumbe huo umerejewa kwa kufafanuliwa wazi kabisa ili kuondosha wasiwasi au kutofahamika kwa matamko hayo. Na mwisho wake muafaka wote umefungwa kwa aya ya mwisho.

  “Nyie muna dini yenu na mimi nina dini yangu”. (Kafiroon:6)

  Inaimaanisha kuwa nyie (makafiri) na mimi Muhammad ni tofauti kabisa na tupo mbalimbali kabisa bila ya kuwepo chochote kati yetu kutuunganisha. Ikhtilafu kamili na ilio wazi kabisa kwa ufahamu wa juu.

  Uislam kwa maana nyingine ni mfumo wa maisha ambao unamuongoza Binaadamu na ulimwengu wote kuelekea kwa Allah (s.w) pekee na kumuekea wazi Binaadamu chanzo cha fikra za dini, sheria, umuhimu, mizani na tabia za kimaisha za binaadamu. Chanzo hicho ni Allah (s.w) na si mwingine. Hivyo maisha yanafatwa kwa kumfuata yeye mola na kuepukana na ushirikina wowote ambao utampelekea binaadamu katika kufuata mfumo mwingine wa kimaisha ambao ni kinyume kabisa na imani ya kiislam.

  Ibn Kathiri kaelezea kuwa uislam umejengeka kikamilifu katika Tauheed ambapo fikra zake, thamani yake, imani yake, na sharia zake zimefunika mambo yote muhimu ya maisha ya binaadamu na yote hayo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na si kwa mwingine. Bila ya kuwepo mzizi huu, tofauti, machafuko, dhana zingeenea. Kwa kuweka wazi katika akili zetu mwenendo wa kiislam usingewezekana kabisa kujengeka katika mawazo au misingi iliyo dhaifu isipokuwa ni lazima ujengeke katika misingi iliyo imara, inyojitegemea, ukweli na uwezo wa kuhimili upinzani wowote uliojengeka kwa muongozo uliowekwa na Allah (s.w).

  “Nyie muna dini yenu na mie nina dini yangu” (Kafiroon:6)

  Hii ndio njia iliofuatwa mwanzo katika kuulingania wito wa Uislam.

  Allah (s.w) ameteremsha sura hii ndani yake amemuamrisha Mtume wake (s.a.w) na pia waisilam wote kwa ujumla, kujiweka mbali na mfumo wa kikifiri wote. Kujiweka mbali na yote ambayo yanatokana na ukafiri. Mtume (s.a.w) na wafuasi wake wanamuabudu Allah (s.w) na lazima waishi kwa kufuata sheria alizoziteremsha mola wao.

  UTIMIZISHAJI WA SURA

  Utimizishaji wa sura hii kwa umma huu wa leo upo katika sehemu nyingi. Allah (s.w) anatukumbusha kwa kusema :

  “Hila ni kitabu tumekuteremshia kwako ni chenye baraka nyingi, ili wapate kuzifikiria aya zake na wenye akili wawaidhike”. (Sad:29)

  1. Tunasoma kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa ijapokuwa katika kukabiliana na mazingira mazito na ugumu wa kulingania uislam, ni lazima turejeshe masuala yetu kwa Allah (s.w) na sheria zake na tusijenge mazingira au matukio ndio marejeo yetu kwa ufumbuzi bila ya kujali hali tunayo ikabili.

  Muafaka waliopewa waisilamu kutoka kwa Makuraishi, katika ulimwengu wa leo unaweza ukafahamika au kulingana na muafaka unaotolewa na Makafiri wa leo kuupa ummati wa kiislam wa leo, jambo la mwanzo la kutimizwa ni kuwa msimamo wetu lazima uwe mmoja uliojengeka kiisilam.

  2. Majibu ya wito wa muafaka wa makafiri wa leo, Allah (s.w) hakuwacha ugumu wowote jinsi ya kujibu wito huo kati ya ukafiri na imani. Bali Allah (s.w) ametuwekea tamko hilo wazi kabisa kutoka katika sura Al-kafiroon, kwa mwenye kujua lugha na asiyeijua lugha hiyo (Kiarabu) ipo wazi kwa kila mtu kufahamu kuwa Allah (s.w) kawaambia Makuraishi na Makafiri wa leo.

  Pia tunaona kuwa mtindo uliotumika katika ujumbe huo ili kutofautisha kati ya Imani na Kufru kuwa ipo wazi kabisa. Pia ni mfumo na sababu ya msingi kwa Waisilamu mpaka siku ya mwisho. Hata sura yenye ikapewa jina la “Sura ya Makafiri.”

  Baada ya tukio la Septemba 11, na kampeni ya hali ya juu dhidi ya Umma wa Kiisilamu ili uwache mfumo wa kimaisha wa Kiisilamu, inatuwekea wazi kwa umma wa Muhammad (saw) ulazima wa kufuata sunna hii ya Mtume na ujumbe wa sura hii, na kuweka wazi jinsia yetu na tofauti kati ya Uisilamu na Ukafiri.

  Kwa nyongeza, linganisha msimamo huu wa Allah (sw) na Mtume wake (saw) na ule msimamo wa viongozi wabovu wa waisilamu hususan wakati wa tukio la Septemba 11.pale Bwana wao Raisi wa Marekani Geoge W. Bush aliposema “..either you are with us or with terrorist..” kumaanisha ya kuwa eitha wapo pamoja na Makafiri katika kuupiga vita Uisilamu au wapo upande wa Waisilamu katika kuupigania Uisilamu. Badala ya kufuata msimamo wa Kiisilamu wamechagua upande wa Kikafiri ukiongozwa na Marekani na kuutupa Uisilamu.

  3. Sura imeweka wazi kuwa Makafiri hawato kubali au kuamini kabisa Uisilamu, Aya nyingi zinaonesha wazi tofauti ya jinsia ya Kiisilamu na Ukafiri. David Blunkett, Waziri wa mambo ya ndani ya Uingereza ameweka wazi msimamo wao aliposema “Wahamiaji (Immigrants) lazima wahakikishe kuwa watoto wao wanakulia kama ni Waingereza” Jumuia ya Waisilamu lazima wafuate mila inayokuabalika nchini” maneno ya David Blunkett.

  Wengi walioingia katika mila hizo miongoni mwa Waisilamu na Makafiri wana hisi kuwa Waisilamu lazima wafuate “mila zanazo kubalika za Kiengereza” au “Mila za Kimagharibi” Baadhi ya watu hao watakufanya uamini kuwa hali hii inakubalika katika Uisilamu. Kwa wote wanao leta wito huo tunawasomea sura hii Al-Kafiroon ili wakumbuke.

  Mwanazuoni Ibn Kathiri amesema kuwa aya hii “Si abudu munavyo viabudu” (Kafiroon:2) ni maneno yanayotiliwa mkazo na aya hii “Na wala sito abudu munavyo viabudu” (Kafiroon:4) “Na wala nyiye hamuabudu ninaye muabudu” (Kafiroon:5), pia imerejewa kwa kuweka wazi zaidi ili iondoshe nafasi yote ya wasiwasi kwa watu au ukosefu wa tafsiri.

  Kwa hivyo vipi iwe ni lazima kwetu sisi Waisilamu tuliokuwa na Haq (Islam), kwa ujinga tu tukubali kuchukuwa fikira za Kikafiri na mfumo wao wa kimaisha na kuwacha Uisilamu, wakati wao hawato kubali kabisa kuacha baadhi tu ya ukafiri wao na kuuchukuwa Uisilamu? NA vipi leo tunawafuata wao kwenye kiza na kuwacha mwangaza (noor na hudaa) kwa makusudi aliyotuteremshia Allah (sw)? Bali sisi ndio wenye Haq (ukweli) na nilazima tuitangaze Haq hiyo (Islam) wazi kwa watu wote.

  4. Kwa uhakika kabisa, kila penye ulinganifu wa Uisilamu (Dawa) kuna ugumu, uzito, machungu na makanusho, na hayo yanapatikana ndani ya mafundisho ya sura hii, kuwa na subira, kushikamana barabara na kamba ya ukweli (Haq) na kuwa imara katika msimamo wetu. Msimamo wetu katika hali hii ni lazima utizame msimamo wa Allah (sw) na Mtume wake (saw) ambao ni..

  “Nyinyi munadini yenu (mwenendo wenu) namimi nina dini yangu (mwenendo wangu)” (kafiroon:6)

  Kimalizio:

  Kwa kumalizia, Sura Al-Kafiroon inatuwekea wazi mafano wa kufuatwa si kwenye histoia ya ulinganiaji (dawa) wa Kiisilamu na ulinganiaji wa Mtume (saw) pekee tu, lakini vile vile ni kwa Ummati huu wa sasa wa Muhammad (saw) pia.

  Kama vile ilivyoteremshwa bila ya kuficha ukweli wake (ujumbe wake) na uzito wa maneno yake kwa makusudio maalumu ya kuaangamiza (kushinda) matumaini yeyote ya Makuraishi wa Makka waliyokuwa nayo wakati huo ilikuubadilisha Uisilamu, msimamo wake na madhara yake lazima yawe sawasawa na mwenedo wa ulinganifu (dawa) wa wakati wetu huu.

  Tofauti tunayo pambana nayo wakati huu ni muhimu sana. Uhitaji wa kufahamu kuwa hakuma nafasi au muda wa kufuata ufumbuzi wa kipindi kifupi au nusu ya ufumbuzi, mapatano (muafaka) au usawazishaji wa mipango. Wito wetu ni wapekee wa Uisilam ambao ni tofauti kabisa na Ukafiri. Lazima tuwakabili watu wa aina hiyo kwa moyo imara na kuwaweka wazi kuwa:

  “Nyiye muna dini yenu (mwenendo wenu) nasi tunadini yetu (mwenendo wetu)” (Kafiroon:6)

  “ Oh Allah ! shuhudia ya kuwa tukefikisha ujumbe wako”

   Similar topics

   -

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 1:19 pm