.


  Nini hatima yangu kwa mungu

  Share

  Anwari

  Posts : 1
  Join date : 2010-08-30

  Nini hatima yangu kwa mungu

  Post  Anwari on Mon Aug 30, 2010 6:07 am

  Hi,

  Shekhe nilikuwa nauliza, Mimi nikijana mwenye umri wa miaka ishirini na 22, natarajia kuoa mwezi huu wa 12 inshallah, ila tatizo ni kwamba mchumba mwenyewe ambae natarajia kuoa ni mkristo, sasa ninalotaka kujua ni kwamba je kuna kizuizi chochote (amaanisha sheria za mungu)amcho kinazuia muislamu kutokuoa mkristo? Lapili. Ni nini hataima yamtu asiefunga hali yakuwa yeye hana tatatizo lolote linlomzuia kutokufunga.

  kwa hayo machache inshallah narajia kupata majibu mazuri inshallah.
  avatar
  BESTY
  Admin

  Posts : 3
  Join date : 2010-08-28
  Location : Here

  Re: Nini hatima yangu kwa mungu

  Post  BESTY on Mon Aug 30, 2010 8:17 am

  Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaah wa Barakaatuh,
  Ndugu katika Iymaan,

  Kwanza tunakumbushana kuwa tunapoandika tuwe tunaanza kwa salaam, na hiyo ndiyo Sunnah na jambo ambalo ni la kuombeana dua Insha'Allah

  JIBU:

  Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

  Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuoa Mkristo. Hakika ni kuwa wapo wengi wasioelewa kuhusu mas-ala ya ndoa baina ya mwanamume Muislamu na mwanamke wa Kitabu. Allaah Aliyetukuka Ametoa ruhusa kwa mwanamume wa Kiislamu kumuoa mwanamke wa Kitabu (Mkristo au Myahudi). Hata hivyo Allaah Aliyetukuka hakuliacha jambo hilo bila ya kuliekea masharti. Ikiwa masharti hayo yaliyowekwa yatakuwa ni yenye kutimizwa basi kutakuwa hakuna tatizo. Aayah inayohusiana na hilo ni ile ya Suratul Maa’idah (5): 5,

  Leo mmehalalishiwa vyote vizuri, na pia chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Na wanawake Waumini Muhswanaat na wale Muhswanaat waliopewa Kitabu kabla yenu ikiwa mtawapatia ujira (mahari) wao kuwataka kwa ndoa wala sio kuweka wazi zinaa wala kuwachukua kama vimada kwa siri”. Neno Muhswanaat lina maana ya wanawake wema watwaharifu waliojiweka mbali na uzinzi. Na ibara za mbele zinamaanisha kuwa wanawake hawa wasiwe ni wale wenye kufanya zinaa kwa siri au dhahiri.

  Ikiwa Mkristo ana sifa hizo basi unaweza kumuoa baada ya kutimiza na hayo masharti mengine ya ndoa. Mbali na kwamba ruhusa hii imetolewa inatakiwa Muislamu awe ni mwenye kujiuliza: Ikiwa kila mwanamme Muislamu anaoa mwanamke wa Kikristo, je hawa wasichana wetu wa Kiislamu wataolewa na nani? Kwa sababu sisi kwa kutotilia maanani hilo leo katika sehemu nyingi wasichana wa Kiislamu wanachukuliwa na Wakristo.


  NB

  Lakini siku hizi kuna khofu kwamba wale wanaooa huenda wakakutana na uovu zaidi. Wanaweza kuwaita katika dini yao na wanaweza kuwalea watoto wao katika Ukristo. Kwa hiyo hatari ipo hakika na ni kubwa. Ili kuwa katika amani, Muumini ni bora asiwaoe. Na katika hali nyingi hakuna uhakika kama mwanamke hatofanya vitendo vya uasharati au hatowaleta watoto waliotoka katika uhusiano wa mwanzo. Lakini mwanamume akitaka kufanya hivyo basi hana dhambi kwake ili ajiweke katika stara na ainamishe macho yake kwa kumuoa. Ajitahidi kumuita katika Uislamu na awe na hadhari na uovu wake na hadhari ya kumruhusu asimvute yeye au watoto wake katika ukafiri". [Fataawa Islaamiyyah, 3/172]

  _______________________________________________________________

  Ama kuhusu swali lako la kuhusiana na kutofunga... Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo katika nguzo za Uislamu, nayo ni wajibu kwa dalili ya kitabu (Qur'an), Sunnah na Ijmai (makubaliano) ya wanavyuoni wote wa Kiislamu.

  1: Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) : Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu. Siku chache tu ( kufunga huko)...(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur'an ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili) Atakae kuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge...(Q2:183-185) .

  2: Na imepokewa hadithi kutoka kwa Abdullah ibn ‘Umar (radhiya Allahu 'anhuma) amesema : Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) akisema: “Umejengwa Uislamu juu ya nguzo tano; kushuhudia ya kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) na kwamba hakika ya Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) ni mtume wa Allah(Subhaanahu wa Ta'ala) na usimamishaji Swalah na utoaji zakah na kuhiji katika nyumba (tukufu) ya alkaaba na funga ya ramadhani. (Al Bukhariy na Muslim).

  Na kuna hadithi nyingine nyingi zinazojulisha wajibu huo, na wanavyuoni wote wamewafikiana juu ya uwajibu huo.


  FADHILA ZA FUNGA

  Zimepokewa Hadithi nyingi sana zinazoelezea fadhila za funga ya Ramadhani, miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi zifuatazo:

  1- Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam): {Mwenye kufunga Ramadhani kwa imani na kutarajia malipo (toka kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) ) husamehewa madhambi aliyoyatanguliza}. (Al Bukhariy na Muslim).

  2- Na amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam): {amesema Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) : Kila amali ya mwanaadamu (aifanyayo) ni yake, wema (mmoja) hulipwa kwa mfano wake mara kumi mpaka mara mia saba, isipokuwa funga, hakika ya funga ni Yangu mimi, na Mimi najua namna gani Nimlipe kwa funga hiyo, ameacha matamanio yake na chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yangu, mfungaji ana furaha mbili, furaha wakati wa kufutari kwake na furaha nyengine pale atapokukutana na Mola wake. Harufu yakinywa cha mfungaji inapendeza zaidi kwa Mwenyezi M ungu kuliko harufu ya miski}. (Al Bukhariy na Muslim).

  3- Alisikika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa Msikitini kwenye Minbar aliitikia Aamiyn, Aamiyn, Aamiyn, Maswahaba wakamuuliza Ya Rasuula Allaah tumekusikia ukiitikia Aamiyn mara tatu;

  “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Alinijia Jibriyl (‘Alayhis Salaam) akaniambia ni khasara iliyoje ya mtu imemfikia Ramadhaan na isiwe ni sababu ya kusamehewa madhambi yake, sema Aamiyn, kisha akanambia ni khasara iliyoje ya mtu aliyewadiriki wazazi wake wawili na isiwe ni sababu ya kuingia Peponi, sema Aamiyn, kisha akanambia ni khasara iliyoje kwa mtu aliyesikia akitajwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha asimswalie, sema Aamiyn.

  Ukweli miongoni mwa watu walio wengi wamekosa msamaha na fadhila za mwezi huu mtukufu, wameacha mafundisho sahihi ya Dini yetu tukufu ya Kiislamu na makosa mengi yanafanywa na wengi wetu.

  NB
  Haikupasi kulipa funga za nyuma zilizompita ulizokuwa huzifungi baada ya kutubu. Hii ni kwa sababu vitendo vyote vya 'ibada kwa Waumini vimewekwa katika muda wake mahsusi uliotajwa. Kwa hiyo ikiwa mtu atawacha kufanya 'ibada hiyo au kuichelewesha na muda upite bila ya sababu yoyote, Allaah سبحانه وتعالى Hatapokea kitendo hicho, na kutokana na hayo, hakuna maana kulipa yaliyompita. Lakini, inampasa atubu kikweli kwa Allaah سبحانه وتعالى na azidishe sana vitendo vyema (kama Sunnah za Swalah, Swawm) na yule mwenye kuomba msamaha kwa Allaah سبحانه وتعالى, basi Allaah Atamsamehe.[b]


  Na Allaah سبحانه وتعالى Ndiye mwenye kujaalia kufuzu.

   Current date/time is Fri Jan 18, 2019 12:45 pm